“Tunatakiwa kuchagua zao moja au mawili na kuyawekeza mkazo
zaidi.Tusiache kulima mazao mengine lakini tuchague mazao machache na
kuyawekea mkazo zaidi” anasema na anaongeza;Tunaweza kuigawa nchi yetu
kimazao. Ikiwezekana kila wilaya ikawa inalima zao fulani. Hii itasaidia kwa sababu hata fedha zikitoka zitajulikana zinakwenda mkoa gani kwa ajili ya kuendelea zao lipi.”
Kwa muda mrefu Serikali imekuwa ikianzisha mipango, sera, miradi na mikakati mbalimbali ya kilimo kwa lengo kuinua uchumi wa Tanzania. Pamoja na kutumia nguvu nyingi, mipango mingi imeshindwa kufikia mafanikio yaliyotarajiwa kutokana na sababu mbalimbali, ikiwamo ya uwepo wa mipango na mikakati mingi kwa wakati mmoja. Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine, Dk Damian Gabagambi anaitaja baadhi ya mipango hiyo kuwa ni Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kuondoa Umaskini (Mkukuta), Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara Tanzania (Mkurabita), Mkakati wa Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDS). Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo (ASDP), Kilimo Kwanza, Uendelezaji Kilimo Ukanda wa Kusini Tanzania (SAGCOT), Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano ambao ulianza mwaka 2011-2016 na Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN). Anasema Tanzania imekuwa ikikwama katika sekta mbalimbali kutokana na kutokuwa na sekta mama ya kuiendeleza kikamilifu kama ilivyo kwa baadhi ya nchi za barani Afrika na Asia. Akizungumza katika warsha ya kuadhimisha siku ya kimataifa ya harakati ya wakulima wadogo na mwaka wa kimataifa wa kilimo cha familia iliyoandaliwa na Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (Mviwata), Dk Gabagambi anasema ili maendeleo yapatikane ni lazima serikali iwe na mpango mmoja itakaousimamia kikamilifu. Anasema kuwa uwepo wa mipango mingi ya kuinua kilimo nchini kwa namna moja au nyingine imekwamisha maendeleo ya kasi katika sekta hiyo.
NINI KIFANYIKE?
Anasema ili kupiga hatua ni lazima Serikali iwe na sekta moja mama, huku akitolea mfano kilimo,kuhakikisha kuwa inaisimamia kikamilifu na kwa muda mrefu ili iweze kufanikiwa. “Mfano ni nchi ya Singapore. Wao walitambua kuwa sekta yao mama ni uvuvi na kuamua kupeleka nguvu zote katika uvuvi,” anasema na anaongeza; “Sekta mama ni ile ambayo ndani ya nchi husika inafanywa na idadi kubwa ya watu. Serikali ikiboresha miundombinu katika sekta hiyo ni lazima itakua na kukuza pato ya nchi.” Anasema kama Tanzania ikiamua kuwa kilimo ndiyo sekta mama,inatakiwa kuweka mazingira rafiki, ikiwa ni pamoja na kuwa na barabara nzuri, maji, umeme na kuhakikisha kuwa inashughulikia ipasavyo migogoro ya ardhi. “Ikiwekeza katika sekta ambayo haina watu wengi uchumi wa nchi husika haiwezi kukua, ukifanya kinyume chake uchumi unaweza kukua lakini wananchi watalia na umaskini maana hawatanufaika na chochote,” anasema. Anasema uchumi unaokuwa bila kuwepo kwa sekta mama, unakuwa siyo kwa ajili ya watu wachache, siyo wote. “Kama ukiwekeza katika kilimo lazima uhakikishe kuwa unawekeza bila kuyumba bila kujali muda wa uwekezaji. Ukipanga miaka 10 au 20ni lazima utaona manufaa ya kilimo”. Anasema uwekezaji wa aina hiyo utachangia kukuza viwanda na kuvutia wawekezaji na ndio njia inayotumiwa na nchi nyingi duniani. “Nchi za China, Vietnam, Malaysia, Thailand, Cambordia zilipiga hatua kimaendeleo kwasababu ya kutambua jambo hili. Nchi hizi hazina wakulima wakubwa zina wakulima wadogo ambao wamewezeshwa kutokana na Serikali za nchi hizo kuwa na kipaumbele kimoja” anasema.
“Tunatakiwa kuchagua zao moja au mawili na kuyawekeza mkazo zaidi. Tusiache kulima mazao mengine lakini tuchague mazao machache na kuyawekea mkazo zaidi” anasema na anaongeza; “Tunaweza kuigawa nchi yetu kimazao. Ikiwezekana kila wilaya ikawa inalima zao fulani. Hii itasaidia kwa sababu hata fedha zikitoka zitajulikana zinakwenda mkoa gani kwa ajili ya kuendelea zao lipi.” Anasema hali hiyo itasaidia kuongezeka kw aidadi ya viwanda nchini na kukaribisha wawekezaji. Kauli ya Serikali Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, George Simbachawene anasema moja ya tatizo linalokwamisha sekta ya kilimo ni migogoro ya ardhi. Anasema hivi sasa wizara yake ipo katika mchakato wa kupima ardhi nchi nzima ili kuondoa migogoro hiyo. “Migogoro hii inachangiwa na viongozi wa ngazi za chini (wenyeviti wa vijiji na watendaji wa kata). Wamekuwa na utaratibu wa kutoa ardhi kwa upendeleo na kwa kutofuata sheria,” anasema na anaongeza; “Serikali itawanyang’anya ardhi watu ambao wameshindwa kuiendeleza ili iwapatie wananchi wenye uwezo wa kuiendeleza. Haiwezekani mtu ahodhi ekari 1,000 bila kuiendeleza wakati kuna wakulima wanataka kufanya shughuli za kilimo.”
Kauli ya Mviwata: Mwenyekiti wa Bodi ya Mviwata, Habib Simbamkuti anasema, “Serikali inatakiwa kuchukua hatua za haraka kumaliza tatizo la ardhi ambalo limekuwa kero na sababu kubwa ya kutopiga hatua katika kilimo. Wakulima wengi nchini hawana ardhi.”
Anafafanua, “Pia inatakiwa kufanya utafiti katika vijiji vyote nchini na kutoa hati za kumiliki ardhi ili kupungua kuenea kwa migogoro yaardhi. Migogoro ya ardhi inayoendelea nchini kati ya wakulima na wawekezaji inasababishwa na ukosefu wa hatimiliki.”
KAULI ZA WAKULIMA
Kauli ya Mviwata: Mwenyekiti wa Bodi ya Mviwata, Habib Simbamkuti anasema, “Serikali inatakiwa kuchukua hatua za haraka kumaliza tatizo la ardhi ambalo limekuwa kero na sababu kubwa ya kutopiga hatua katika kilimo. Wakulima wengi nchini hawana ardhi.”
Anafafanua, “Pia inatakiwa kufanya utafiti katika vijiji vyote nchini na kutoa hati za kumiliki ardhi ili kupungua kuenea kwa migogoro yaardhi. Migogoro ya ardhi inayoendelea nchini kati ya wakulima na wawekezaji inasababishwa na ukosefu wa hatimiliki.”
KAULI ZA WAKULIMA
Wakieleza matatizo wanayokumbana nayo wakulima, Ashura Magendo ambaye ni Ofisa Mtendaji kijiji cha Muhaga Kata ya Kibute wilayani Kisarawe mkoani Pwani, anasema wakulima wa kijiji hulima zaidi mihogo lakini hivi sasa wanashindwa kuendesha kilimo hicho kutokana na mimea kuliwa na wadudu. “Miaka ya nyuma walikuwa wanalima eka tano hadi 20 na kila eka walikuwa wakipata zaidi ya Sh1 milioni. Lakini kutokana na magonjwa hayo hivi sasa wanapata kati ya Sh10,000 hadi 50,000 kwaeka kutokana na mihogo kuoza”. Anasema wataalamu wa kilimo walipofika katika kijiji hicho waliwaeleza kuwa wadudu hao wanasababishwa na mimea ya Mbono Kaburi ambao huzalisha nishati ya mafuta yanayotumiwa kuendeshea mitambo viwandani. Naye Mohamed Rashid ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Chakenge Kata ya Mzenga wilayani Kisarawe anasema kuwa kijiji hicho ni miongoni mwa vijiji 11 vilivyotoa ardhi kwa ajili ya kilimo cha Mbono Kaburi. Anasema wakati wa utoaji wa ardhi watu ambao walikuwa na maeneo katika shamba hilo walitakiwa kulipwa fidia ambayo haikulipwa kwa wakati, hata waliolipwa walipunjwa. “Tangu mwaka 2008 tulipaswa kulipwa lakini fedha za kulipwa ambazo ni Sh500 milioni zilitolewa mwaka 2012. Watu wengi waliolipwa walipata fedha kidogo kuliko uhalisia” anasema na kuongeza kuwa ili Tanzania iweze kuwa na maendeleo ya kasi ni lazima kuwa na tabia ya kufanya ahadi kwa vitendo.








0 comments:
Post a Comment